SARATANI YA TEZI DUME NININI?
Tezi dume ni tezi inayopatikana kwa jinsia ya kiume. Tezi hii ina kazi ya kutengezeza majimaji meupe mepesi yenye unato kidogo. Majimaji haya husaidia mbegu za kiume kutembea kwa urahisi.
Ipo wapi?
Tezi dume iko mwishoni mwa kibofu cha mkojo. Pia inauzunguks mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na na mrija wa mkojo wa uume (urethra) na iko mbele kidogo ya utumbo mpana ndani ya fupa la nyonga.
Saratani ya tezi dume ni nini?
Saratani ya tezi dume maana yake ni tezi dume imepata ugonjwa wa saratani..Na hii hutokea pale ambapo chembechembe hai za tezi huasi na kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili, chembechembe asi hizi mwishowe hutengeneza vivimbe hatari ndani ya tezi dume na hatimaye husambaa mwilini
Visababishi hatarishi kwa saratani ya Tezi dume
Umri Mkubwa kuanzia miaka 50
Nasaba (ukoo wenye historia a saratani hii
Lishe hatarishi-nyama nyekundu kwa wingi, mafuta/samli,maziwa ya krimu
Unene uliokithiri
Ukosefu wa mazoezi
Upungufu wa virutubisho,mfano vit D.
Maambukizi ya mara kwa mara kwenye tezi dume
Dalili zake ni zipi?
Udhaifu katika utoaji wa mkojo, mkojo hauishi.
Kwenda kukojoa mara kwa mara.
Damu ndani ya mkojo.
Kushindwa kukojoa.
Maumivu ya kiuno na mifupa ya nyonga.
Wagonjwa wengi huanza maumivu ya nyonga kama ni dalili za awali.
Udhaifu katika utoaji wa mkojo pia kunaweza kutokea kwa kuvimba kwa tezi dume bila ya saratani.
Damu kwenye mkojo nakushindwa kumaliza mkojo ni ishara tosha ya kuwa tezi dume imeathirika.
UCHUNGUZI
Wanaume wote wanpaswa kufanya uchunguzi wa saratani ya tezi dume kuanzia miaka 50. Kwa wale wenye historia katika familia wanapaswa kuanza wakiwa na umri wa miaka 45.
Uchunguzi unafanyika kwa njia zifuatazo
Uchunguzi kwa cancer marker kwa kuchunguza damu (PSA).
Uchunguzi kwa njia ya kipimo cha njia ya haja kubwa (DRE)
Biopsy.
Ultrasound.
X-ray.
Bone scan.
Jinsi ya kutibu saratani ya tezi dume
Upasuaji.
Mionzi
Dawa ya saratani
Homoni.
Matibabu hutegemea
Ngazi na ukali wa ugonjwa.
Je, ugonjwa upo ndani ya tezi dume tu au umesambaa.
Umri na afya ya mgonjwa.
Magonjwa ambatanishi na saratani hiyo, shinikizo la damu, matatizo ya moyo na kisukari.
TIBA
UPASUAJI
Kuondoa tezi dume yote peke yake inaweza ikatosha.
Kuondoa tezi dume na tezi jirani.
Kuondoa tezi dume na kuhasi
Kuondoa tezi dume kidogo kupitia njia ya mkojo na kumpa mgonjwa tiba shufa.
MIONZI.
Sawa na upasuaji inaweza kuondoa ugonjwa iwapo haujasambaa.
Mionzi pia hutolewa kama tiba shufaa.
DAWA YA SARATANI
Baadhi ya wagonjwa hufaidika na tiba hii, dawa hutolewa kwa muda mfupi na kufuatilia maendeleo ya mgomjwa kwa kufanya PSA,dawa inaweza kuwa moja au mchanganyiko.
HOMONI
Hutolewa mfullulizo kwa njia ya vidonge au sindano.
Ufuatiliaji wa karibu
Ni muhimu kufuatilia hali ya tezi isirejee baada ya ugonjwa kutibiwa kwa kufanya kipimo cha PSA mara kwa mara angalau miezi mitatu mara moja.
Athari zitokanazo na matibabu mbalimbali yaliyotajwa.
Upasuaji
Unaweza kusababisha kutoweza:
🔥🔥🔥Kuzuia mkojo
Kupoteza nguvu za kiume.
Homoni
Homoni huongeza joto mwilini
Kupungukiwa na nguvu za kiume
CHUKUA TAHADHARI KABLA YA HATARi📲:+255746641655
0 Comments