SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

   Sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni nyingi lakini kwa ujumla karibu zote tunaweza kuzigawanya katika makundi manne:

1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme

Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme. Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke. Mwanamke atakosa hamu ya kufanya mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na kama atahisi kuna ukosefu wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.

2. Matatizo Katika Maisha Yako;

Matatizo mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:

Matatizo Katika Kufanya Tendo La ndoa;

Kama mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au kama mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo ya afya

Magonjwa mengi husababisha mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni maumivu ya viungo vya mifupa (arthritis), kansa, ugonjwa wa kisukari, high blood pressure, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na matatizo ya akili.

Matumizi ya madawa

Baadhi ya madawa yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.


Mtindo wa maisha;

Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.

Upasuaji;

Upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au katika maeneo ya viungo vya uzazi humbadilishia mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.

Uchovu: 

Unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe huweza kuathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.

3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa Homoni.

Kukoma hedhi:  Mabadilko ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa homoni hiyo husababisha uyabisi wa viungo vya sehemu nyeti na kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone, homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.

Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.

Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

4. Matatizo Ya Kisaikolojia

Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:

 Wasiwasi na kuwa na msongo wa mawazo

 Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi

 Kuhisi kutothaminiwa katika jamii

 Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa  au kubakwa

 Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi.

KAMA WEWE NI MWANAMKE UNAE PITIA CHANGAMOTO HII PATA SULUHISHO SAHIHI SASA:

📲+255746641655 call/wattsap

Au bonyeza link hii kuja wattsap in box👉https://bit.ly/3XgpzOD