Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum, ambaye pia huitwa spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko. Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini inayotanda kwenye midomo au sehemu nyeti.
Mwanamke mwenye mimba na ana ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni kupitia placenta au wakati wa kuzaliwa. Aina hii ya kaswende huitwa congenital syphilis, na inaweza kusababisha kujifungua mtoto mfu au mtoto akafa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Watoto wengi hawaonyeshi dalili wanapozaliwa. Baadaye watoto huota vijipele, hupata matatizo ya meno, na kubonyea kwa mfupa wa pua – hali inayoitwa saddle nose, kuwa viziwi, kuwa na watoto wa jicho na kifafa.
Dalili Za Kaswende
Kuna hatua nne za ugonjwa huu wa kaswende. Ni dalili gani utaziona, inategemeanan na ugonjwa upo katika hatua ipi katika hizi nne. Hatua hizi zinaweza kuingiliana na dalili si lazima zitokee kwa mtiririko ule ule. Unaweza pia ikawa na kaswende na usione dalili zo zote kwa miaka kadhaa.
Lakini, hata kama hujaona dalili zo zote, bado unaweza kumwambukiza mpenzi wako.
Hatua Ya kwanza Ya Kaswende – Primary Syphilis
Dalili za hatua ya kwanza huonekana siku 10 hadi miezi 3 baada ya kuambukizwa. Unaweza pia kuona mitoki maeneo ya kinena chako.
Mara nyingi, dalili ya kwanza kabisa imayoonekana ni aina ya mchubuko mdogo, mgumu usio na maumivu (chancre) juu ya ngozi (unaweza ukatokewa na michubuko zaidi ya mmoja). Mchubuko huu aghalabu hutokea pahala ambapo bakteria waliingilia. Ni mchubuko usio na maumivu, na unaweza kutokea sehemu ya uficho kama kwenye uke au ndani ya rektamu. Unaweza usijue kama una mchubuko huu.
Mchubuko huu utapona wenyewe katika wiki 3 hadi 6. Haimaanishi kuwa umepona. Maana yake ni kwamba unaingia hatua ya pili ya ugonjwa wa kaswende.
Hatua Ya Pili Ya Kaswende – Secondary Syphilis
Wiki 2 hadi 10 baada ya mchubuko wa kwanza kutokea, unaweza kuona dalili zifuatazo:
. Vipele vidogo mwilini, vya mviringo vyenge rangi ya nyekundu au vyenye wekundu wa kahawia. vijipele huota mara nyingi vikianzia mgongoni na kuenea mwili mzima, pamoja na kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo.
. Michubuko inayofanana na chunjua huotokea mdomoni, ukeni au kwenye mkundu
. Homa
. Kuvimba tezi
. Kukonda
. Kupunyuka nywele
. Kuumwa kichwa
. Uchovu mkali
. Maumivu ya misuli
Tiba sahihi isipotolewa, ugonjwa utatoweka tena na kurudi tena baadaye, mara nyingi baada ya mwaka mmoja. Hata kama dalili hazionekani, ugonjwa bado upo na unazidi kuwa mbaya zaidi, na unaweza kumwambukiza mwenzi wako.
Michubuko inayofanana na chunjua hutokea kwenye sehemu za midomo na mkundu. Vile vile kutatokea maumivu ya misuli, homa, kukauka koo, kuvimba tezi, kupunyuka nywele, kukonda na uchovu wa mwili.
Latent Syphilis
Kama tiba ya kaswende ya hatua ya pili haitatolewa, ugonjwa utaendelea kwenye hatua iitwayo latent stage. Katika hatua hii inayoweza kudumu kwa miaka kadhaa, mwili utautunza ugonjwa bila kuonyesha dalili zo zote. Pamoja na kuwa hakuna dalili zo zote zitakazoonekana, ugonjwa huu unaweza kuendelea kwenye hatua ya mwisho.
Hatua Ya Tatu Ya Kaswende – Tertiary syphilis
Asilimia 15 ya watu ambao hawakupata tiba kwenye hatua ya pili ya kaswende watapata kaswende ya hatua ya tatu – tertiary syphilis.
Hii ni hatua ya mwisho, na mbaya zaidi ya zote. Hatua hii hutokea miaka 10 hadi 30 baada ya maambukizi ya awali. Unaweza kupata ulemavu wa kudumu wa kiungo cha mwili au kifo. Madhara yanaweza kuwa:
. Matatizo ya kwenye ubongo
. Kiharusi
. Maambukizi kwenye ngozi laini inayouzunguka ubongo au uti wa mgongo
. Ganzi
. Ukiziwi
. Kutoona vizuri au upofu
. Usahaulifu (dementia)
. Matatizo ya valvu za moyo
. Aneurysm
. Magonjwa ya mishipa ya damu
KWA ELIMU ZAIDI NA SULUHISHO SAHIHI JUU YA AFYA YA UZAZI NA SAYANSI YA TENDO LA NDOA {Kuludisha nguvu za kiume na kukosa hisia kwa wanawake,matatizo ya hedgi,kukusa ute ute ukeni kushindwa kushika ujauzito}CONTACT📲;+255746641655
Au bonyeza link hii kuja inbox wattsap👉https://bit.ly/3XgpzOD
0 Comments