VIJITI/KIPANDIKIZI
Vijiti ni nini?
Hii ni moja ya njia ya uzazi wa mpango ambayo kipande kidogo chembamba cha plastiki ambacho kinakua na homoni ya progesterone kinawekwa ndani ya mkono wa juu.
Upasuaji mdogo usio na maumivu hufanyika kuweka vijiti hivyo..
Aina za vijiti..
Kuna aina kuu mbili za vijiti ambazo ni.
· Implanon:
Hii ni aina ya kijiti ambayo huwekwa moja kwenye mkono na huzuia mimba kwa uhakika kwa mda wa miaka miatatu.
· Jadelle:
Hii ni aina ya vijiti ambavyo huwekwa viwili kwa wakati mmoja na huweza kuzuia mimba kwa mda wa miaka mitano.
Jinsi vijiti vinavyofanya kazi..
· Huzuia mayai kutoka kwenye ovari kushuka kwenye mfuko wa uzazi kukutana na mbegu za kiume.
· Huongeza utepe kwenye mlango wa uzazi kuzuia mbegu za kiume kuingia kwenye mfuko wa uzazi..
Faida za kutumia vijiti kama uzazi wa mpango..
· Huzuia kupungua kwa wingi wa damu{iron dificiency anaemia} kwasababu huzuia damu ya kila mwezi kutoka.
· Haiharibu au kupunguza ubora wa maziwa.
· Ni njia ya uhakika.
· Inazuia mimba kwa miaka mingi.
· Sio rahisi mtu mwingine kufahamu kama unatumia njia hiyo.
ukitoa kijiti tu unaweza kubeba mimba kwa mda mfupi..
Madhara madogo madogo ya njia hiyo ya uzazi wa mpango.
· Kubadilika kwa mfumo wa kutoka damu mwisho wa mwezi kama kutoka damu nyingi sana, matone ya damu au kukata kabisa kwa damu.
· Maumivu ya tumbo na kichwa..
· Maumivu ya matiti,
· Kuongezeka uzito.
· Kuongezeka au kuisha kabisa kabisa kwa chunusi.
Mwisho: hii ni moja ya njia bora zaidi za uzazi wa mpango kwasababu haina usumbufu kabisa mpaka miaka mitatu au mitano iishe lakini unaruhusiwa kuondoa kama ukihitaji mototo kabla mda uliopangwa haujaisha.
Ukipata matatizo yeyote makubwa muone daktari haraka..
KWA ELIMU ZAIDI NA USHAULI📲+255746641655
By Dr.Simfukwe🔬💊💉
0 Comments